Kwa sasa TZ-CERT inatoa huduma zifuatazo kwa washirika na umma kwa jumla.
(i) Tahadhari na Onyo
Kutokana na kukua kwa matishio ya usalama mtandaoni, TZ_ZERT wakati wote inafuatilia matishio ya kiusalama ya mtandao na uwezekano wa kudhuriwa na kuweza kushauri washirika na umma kwa jumla.
(ii) Mwitikio wa Tukio
Kwa utaalam wa usalama wa mtandao, TZ-CERT yaweza sasa kufanya kazi na asasi za washirika kuitikia kwa matukio yote ya kiusalama ya mtandao katika mitandao yao mahususi. Pamoja na hayo TZ-CERT inatoa msaada wa hatua kwa hatua kwa asasi inayokabiliwa na mashambulio ya kiusalama.
(iii) Mwamko wa Usalama wa Mtandao
Ikiwa na jukumu la kuboresha usalama wa mtandao nchini, TZ-CERT inafanya kazi ya kusambaza taarifa za kiusalama wa mtandao kwa jamii. Hii inajumuisha kuendeleza utendaji wa mfano kwa watumiaji wa teknolojia.
TZ-CERT itaboresha huduma zake na kulenga utoaji wa huduma nyingine za mtandao kwa jamii ikiwemo Ukaguzi wa usalama na tathmini, Uchambuzi wa mifumo tumizi haribifu,Ugunduzi wa kuingiliwa, Uchambuzi wa hatari na Ushauri wa Usalama.