A huge collection of 3400+ free website templates JAR theme com WP themes and more at the biggest community-driven free web design site
Give your website a premium touchup with these free WordPress themes using responsive design, seo friendly designs www.bigtheme.net/wordpress
Home / Kuhusu Sisi / Wasifu wa TZ-CERT

Wasifu wa TZ-CERT

Timu ya Mwitikio wa Kukabili Majanga ya Kompyuta Tanzania, kwa kifupi TZ-CERT,  ni timu yenye jukumu la kuratibu mwitikio wa  matukio ya usalama wa mtandao  ngazi ya taifana kushirikiana na vyombo vingine vya kikanda na kimataifa  vinavyojishughulisha na usimamizi wa matukio ya kiusalama wa  mtandao.   TZ-CERT ilianzishwa chini ya Kifungu 124 cha Sheria ya Elektroni na Posta (EPOCA) Na. 3 ya 2010 ndani ya mfumo wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).

Dira Yetu
Kuwa kiungo kinachoaminiwa duniani kote cha kushughulikia matukio ya kiusalamawa mtandao.

Dhamira Yetu
Kuboresha na kuunga mkono msimamo wa taifa kuhusu usalama wa mtandao,  kuratibu ushirikiano wa taarifa na kwa makusudi kusimamia mashaka ya mtandao  wakati huo huo kusaidia ahadizawashirika.

Lengo Letu
Lengo kuu la CERT ya Taifa ni kuwa na usalama  wa hali ya juu na wa uhakika ndani ya nchi;  na kujenga utamaduni wa usalama wa mtandao na taarifa  kwa manufaa ya jamii (serikali, wananchi, walaji, biashara na asasi za sekta ya umma) na hivyo kuchangia utendaji kazi usio na vikwazo  wa shughuli zinazoendelea mtandaoni.