A huge collection of 3400+ free website templates JAR theme com WP themes and more at the biggest community-driven free web design site
Give your website a premium touchup with these free WordPress themes using responsive design, seo friendly designs www.bigtheme.net/wordpress
Home / Maswali yanayoulizwa mara kwa mara

Maswali yanayoulizwa mara kwa mara

SWALI : JE TZ-CERT  NI NINI?

TZ_CERT ni kifupisho cha Tanzania Computer Emergency Response Team, timu ya kitaifa yenye wajibu wa kuratibu mwitikio wa matukio ya usalama wa kimtandao katika ngazi ya Taifa na kushirikiana na vyombo vya kikanda na vya kimataifa vinavyoshughulikia udhibiti wa matukio ya usalama  wa kimtandao.

SWALI :  JE, NANI ANAYESIMAMIA TZ-CERT?

TZ-CERT iko ndani ya muundo wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA)

SWALI : JE, TZ-CERT INAFANYA NINI?

1.    Inatoa fursa ya kutoa taarifa ya matukio ya usalama wa kompyuta yatakayopitiwa na kushughulikiwa.
2.    Inasambazaa taarifa za matukio muhimu yanayohusu  umma.
3.    Inaleta utambuzi wa usalama wa mtandao.

SWALI : JE, NI MATUKIO GANI  YA MARA KWA MARA YA USALAMA WA KOMPYUTA?

Linaweza kuwa tukio la kweli au  linalotuhumiwa lenye madhara kuhusiana na usalama wa mifumo ya kompyuta au  mitandao ya kompyuta katika kukiuka wazi wazi au kudhaniwa kukiuka sera ya usalama wa kompyuta. Matukio hayo yanaweza kujumuisha shughuli kama vile :
1.    Kujaribu  kuingia bila idhini  kwenye mfumo au data zake
2.    Kukatiza kusikotakiwa au kunyimwa huduma
3.    Kutumia mfumo kusikoidhinishwa  kwa ajili ya kuchakata au kuhifadhi data
4.    Kubadili vifaa vya mfumo, programu tumizi zinazodhibiti na kusimamia, au sifa bainifu za programu tumizi bila ya idhini, taarifa au maelekezo ya mmiliki.

SWALI : JE, NI NANI WATATOA TAARIFA ZA MATUKIO YA USALAMA WA KOMPYUTA?

Washirika wa TZ-CERT, watu au taasisi ambazo TZ-CERT imekusudiwa kuwahudumia au kuwasaidia ambao ni pamoja na :
1.    Serikali
2.    Miundombinu muhimu ya TEHAMA
3.    Ulinzi na Usalama
4.    Taasisi za fedha na benki
5.    Taasisi  za kitaaluma
6.    Wananchi kwa jumla

Swali : Je, utatoaje taarifa ya matukio kwa TZ-CERT?

Matukio yanaweza kutolewa taarifa kwa TZ-CERT kupitia :-

Fomu ya utoaji taarifa ya tukio :  www.tz-cert.go.tz
Barua pepe : incidents@tzcert.go.tz
Simu : +255 22 2412039
Faksi : +255 22 2412038

Swali : JE, NINI SAA ZA KAZI ZA TZ-CERT

Ofisi za TZ-CERT ziko wazi kuanzia Jumatatu hadi Ijumaa saa 2 asubuhi hadi 10 jioni.

Maswali na mapendekezo yanakaribishwa. Tafadhali tuandikie barua pepe kupitia   info@tzcert.go.tz